• HABARI MPYA

    Monday, June 08, 2015

    KADO, NIZAR WATUA MWADUI FC, ‘CHAMA’ LA JULIO LITATISHA LIGI KUU MSIMU UJAO

    Na Philipo Chimi, SHINYANGA
    MWADUI FC ya Shinyanga imefanikiwa kumsajili kipa wa zamani wa Yanga SC, Shaaban Hassan Kado ambaye hivi karibuni aliachwa na klabu yake, Coastal Union ya Tanga.
    Wageni hao katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Mwadui FC ya Shinyanga wanaonekana kupania kuwa washindani wazuri wa ubingwa msimu ujao.
    Mbali na kufanikiwa kumbakiza kocha wake Jamhuri Mussa Kihwelo ‘Julio’ na wachezaji nyota waliopandisha timu hiyo, Mwadui imekamilisha usajili wa nyota wengine kadhaa wenye uzoefu.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY leo, Katibu Mkuu wa Mwadui, Ramadhani Crao amesema wamewasajili kipa Kado na kiungo wa Yanga SC, Nizar Kalfhan, ambaye anakwenda kuungana na mdogo wake, Razack Khalfan aliyewahi kuchezea Yanga SC pia.
    Kutoka kulia Shaaban Kado, Razack Khalfan na Nizar Khalfan ambao wote ni wachezaji wa Mwadui 

    Tayari Mwadui yenye maskani yake Kishapu, ilikuwa imekwishakamilisha usajili wa nyota wengine kama beki Anthony Matogolo na washambuliaji Paul Nonga kutoka Mbeya City na Rashid Mandawa wa Kagera Sugar. 
    Timu hiyo inatarajiwa kuanza mazoezi Juni 15, mwaka huu kujiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inayotarajiwa kuanza Agosti mwaka huu.
    Mwadui FC ni kati ya timu nne zilizopanda Ligi Kuu msimu ujao, nyingine zikiwa ni Toto Africans ya Mwanza, Majimaji ya Songea na African Sport ya Tanga.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KADO, NIZAR WATUA MWADUI FC, ‘CHAMA’ LA JULIO LITATISHA LIGI KUU MSIMU UJAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top