• HABARI MPYA

    Wednesday, August 13, 2014

    TFF HAITAMBUI MABADILIKO YA UONGOZI COASTAL UNION

    Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesema halitambui mabadiliko ya uongozi ndani ya Coastal Union yanayodaiwa kufanywa na mkutano wa wanachama wa klabu hiyo uliofanyika hivi karibuni.
    TFF imesema uongozi wa Coastal Union uliochaguliwa na mkutano wa uchaguzi wa klabu hiyo ndiyo ambao wanautambua, na wataendelea kufanya nao kazi, na sio uongozi mwingine wowote ule.
    Rais wa TFF, Jamal Malinzi kulia akiwa na Rais wa FIFA, Sepp Blatter

    “Tunapenda kuwakumbusha wanachama wetu (ikiwemo Coastal Union) kuheshimu katiba ya TFF pamoja na katiba zao, kwani hazitambui mapinduzi ya uongozi wala kamati za muda za utendaji. TFF inafanya kazi za kamati za utendaji zilizopatikana kwa njia ya uchaguzi tu,”.
    “Tayari tumepokea barua kutoka kwa Kaimu Mwenyekiti wa Coastal Union, Steven Mnguto ikilalamikia kusimamishwa kwake,”.
    “Hivyo, tunafuatilia suala hilo kwa kina, na ikibainika kuwa kuna viongozi wamehusika katika mapinduzi hayo watafikishwa katika vyombo husika kwa hatua zaidi,”imesema taarifa ya TFF.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF HAITAMBUI MABADILIKO YA UONGOZI COASTAL UNION Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top