• HABARI MPYA

    Monday, August 11, 2014

    MIROSLAV KLOSE ASTAAFU UJERUMANI BAADA YA REKODI YA KUTISHA YA MABAO HADI KOMBE LA DUNIA

    MFUNGAJI bora wa kihistoria wa Ujerumani, Miroslav Klose, ametangaza kustaafu soka ya kimataifa.
    Kiasi kama cha mwezi mmoja tangu ashjinde Kombe la Dunia na nchi yake nchini Brazil, mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 36 ameamua kupumzika timu ya taifa.
    Amefikisha jumla ya mabao 16 aliyofunga katika Kombe la Dunia na jumla ameifungia mabao 71 timu yake ya taifa. Huyo ndiye pia mfungaji wa mabao mengi zaidi katika Fainali za Kombe la Dunia, akifuatiwa na Mbrazil Ronaldo Lima mwenye mabao 15. 
    Mchezo umekwisha: Miroslav Klose ametangaza kustaafu soka ya kimataifa baada ya kuifungia Ujerumani mabao 71

    REKODI YA MABAO YA KLOSE KOMBE LA DUNIA

    1, 2, 3: Ujerumani 8-0 Saudi Arabia, makundi, 2002
    4: Ujerumani 1-1 Jamhuri ya Ireland, makundi, 2002
    5: Cameroon 0-2 Ujerumani, makundi, 2002
    6, 7: Ujerumani 4-2 Costa Rica, makundi, 2006
    8, 9: Ecuador 0-3 Ujerumani, makundi, 2006
    10: Ujerumani 1-1 Argentina (baada ya dakika 120, penalti 4-2), Robo Fainali, 2002
    11: Ujerumani 4-0 Australia, makundi, 2010
    12: Ujerumani 4-1 England, 16 Bora, 2010
    13, 14: Argentina 0-4 Ujerumani, Robo Fainali, 2010
    15: Ujerumani 2-2 Ghana, makundi, 2014
    16: Brazil 1-7 Ujerumani, Nusu Fainali, 2014
    Perfect ending: Klose scored twice as Germany lifted the World Cup in Brazil this summer
    Klose alifunga mabao mawili Ujerumani ikitwaa Kombe la Dunia nchini Brazil mwaka huu
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MIROSLAV KLOSE ASTAAFU UJERUMANI BAADA YA REKODI YA KUTISHA YA MABAO HADI KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top