KLABU ya Manchester City imethibitisha kukamilisha usajili wa Eliaquim Mangala kutoka Porto, na mchezaji huyo amesema anataka kushinda mataji na mabingwa hao wa England.
Man City ambayo inakamilisha usajili wa mchezaji huyo siku moja baada ya kufungwa na Arsenal mabao 3-0 katika mechi ya Ngao ya Jamii, inaaminika wamelipa Pauni Milioni 32 kumpata mchezaji huyo.
Beki huyo wa kati atavaa jezi namba 20 Uwanja wa Etihad, na pia amesema kusajiliwa kwa mchezaji mwenzake wa Porto, Fernando Man City kumesaidia.
Kifaa kipya: Eliaquim Mangala baada ya kusaini Manchester City
0 comments:
Post a Comment