• HABARI MPYA

    Monday, August 11, 2014

    FERDINAND ASAINI MIAKA MIWILI READING

    BEKI Anton Ferdinand amesaini mkataba wa miaka miwili na Reading baada ya mwaka mmoja wa kutemwa na Queens Park Rangers.
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 alikuwa akiichezea Antalyaspor lakini ameamua kuondoka Uturuki na kurudi nyumbani. Ilifikiriwa kwamba mdogo huyo wa Rio, aliyewahi kuchezea West Ham alikuwa tayari kusaini Mkataba na Polisi United ya Thailand, lakini akaamua kurejea England. 
    "Nimekuwa mbali na soka ya England kwa mwaka na nimekuwa na wakati fulani mgumu,"amesema Ferdinand. "Uturuki ni sehemu nzuri kwenda na kucheza soka, lakini mambo fulani nje ya Uwanja hayakunipa fursa ya kucheza soka yangu haswa,". 

    Amerudi nyumbani: Beki wa zamani wa QPR, Anton Ferdinand akiwa ameshika jezi ya Reading baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FERDINAND ASAINI MIAKA MIWILI READING Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top