• HABARI MPYA

    Sunday, August 10, 2014

    ARSENAL WABEBA NGAO YA JAMII BAADA YA KUIBUTUA MAN CITY 3-0

    ARSENAL imebeba Ngao ya Jamii baada ya kuwafumua mabingwa wa Ligi Kuu ya England, Manchester City mabao 3-0 jioni hii Uwanja wa Wembley, London.
    Katika mchezo huo wa kuashiria ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu ya England, mabao ya The Gunners yamefungwa na Santi Cazorla dakika ya 21, Aaron Ramsey dakika ya 42 na Olivier Giroud dakika ya 60.
    Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Szczesny, Debuchy, Chambers, Koscielny/Monreal dk46, Gibbs, Arteta, Sanchez/Oxlade-Chamberlain dk46, Ramsey/Campbell dk86, Wilshere/Flamini dk68, Cazorla/Rosicky dk70 na Sanogo/Giroud dk46.
    Man City: Caballero, Clichy, Boyata, Nastasic, Kolarov/Richards dk76, Navas/Sinclair dk85, Toure/Milner dk60, Fernando, Nasri/Silva dk46, Dzeko/Zuculini dk60 na Jovetic.

    Hivi ndivyo tunavyouanza msimu! Santi Cazorla akiruka juu kushangilia bao lake katika mechi ya Ngao ya Jamii
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ARSENAL WABEBA NGAO YA JAMII BAADA YA KUIBUTUA MAN CITY 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top