• HABARI MPYA

    Thursday, July 10, 2014

    SIRI YAFICHUKA, KUMBE WACHEZAJI UHOLANZI WALIMGOMEA VAN GAAL KUPIGA PENALTI

    KOCHA wa Uholanzi, Louis van Gaal amesema kwamba wachezaji wake wawili waligoma kupiga penalti ya kwanza jana wakitolewa na Argentina Katika Nusu Fainali Kombe la Dunia.
    Uholanzi ilishindwa kurudia ilichokifanya Robo Fainali dhidi ya Costa Rica waliposhinda kwa penalti, baada ya beki wa Aston Villa, Ron Vlaar kukosa penalti ya kwanza na Wesley Sneijder pia akapoteza.
    Mzaha: Kipa Sergio Romero akiokoa penalti ya Ron Vlaar wa Uholanzi

    Argentina ilifunga penalti zote nne kujihakikishia kutinga Fainali ambako itamenyana na Ujerumani Uwanja wa Maracana Jumapili.
    Baada ya mechi, Van Gaal - ambaye anakwenda kuanza kazi Manchester United wiki ijayo- alisema kwamba wachezaji wake wawili waligoma kupiga penalti ya kwanza.
    "Unahitaji kufunga ya kwanza na niliwaomba wachezaji wawili kupiga mpira wa kwanza, nikamalizia na Vlaar. Nafikiri alikuwa mchezaji bora uwanjani, hivyo alikuwa anajiamini. Ikaonekana si rahisi kufunga katika matuta,"amesema.
    Acrobatic: Argentina goalkeeper Sergio Romero saves a penalty from midfielder Wesley Sneijder
    Mkali wa matuta: Kipa wa Argentina, Sergio Romero akiokoa penalti ya kiungo Wesley Sneijder
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIRI YAFICHUKA, KUMBE WACHEZAJI UHOLANZI WALIMGOMEA VAN GAAL KUPIGA PENALTI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top