• HABARI MPYA

    Thursday, July 10, 2014

    ORIGI ATUA LIVERPOOL KUKAMILISHA USAJILI

    KLABU ya Liverpool iko mbioni kukamilisha usajili wa wachezaji wawili wa kimataifa wa Ubelgiji kwa Pauni Milioni 30, Divock Origi na winga wa Benfica, Lazar Markovic.
    Origi mwenye asili ya Kenya, aliyeichezea Ubelgiji Kombe la Dunia mwaka huu Brazil, alipigwa picha wakati anawasili Liverpool Jumatano hii kujadili vipengele vya Mkataba na viongozi wa Wekundu hao viwanja vya mazoezi vya timu hiyo, Melwood na anaweza kwenda kufanyiwa vipimo Alhamisi hii pamoja na Markovic.
    Ada ya Pauni Milioni 19.8 kwa ajili ya Markovic inaaminika imekubaliwa na Benfica - wakati Origi ataondoka Lille ya Ufaransa kwa Pauni Milioni 10, ingawa Tottenham nato imetupa ndoana zake kwa mshambuliaji huyo Kibelgiji.

    Wanatua Anfield? Divock Origi (kulia) amesafiri kwenda Liverpool kujadili Mkataba na klabu hiyo tayari kujiunga nayo
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ORIGI ATUA LIVERPOOL KUKAMILISHA USAJILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top