• HABARI MPYA

    Monday, July 14, 2014

    MESSI MCHEZAJI BORA KOMBE LA DUNIA 2014, NEUER KIPA BORA

    LIONEL Messi amepoza machungu kidogo baada ya kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Kombe la Dunia 2014.
    Nyota huyo wa Barcelona ameshindwa kuisaidia Argentina kutwaa Kombe la Dunia baada ya kufungwa 1-0 na Ujerumani katika Fainali 
    Uwanja wa Maracana mjini Rio de Jeneiro, Brazil.  
    Bao hilo pekee la Ujerumani, lilifungwa na Mario Gotze aliyeingia kuchukua nafasi ya Miroslav Klose dakika 88, aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 112.

    Messi kulia akiwa na tuzo yake na kushoto ni Manuel Neuer akiwa na tuzo yake ya kipa bora
    Mlinda mlango wa Ujerumani, Manuel Neuer ameshinda tuzo ya kipa bora wa mashindano ya mwaka huu, ambayo wenyeji Brazil wameambulia nafasi ya nne baada ya kufungwa 3-0 na Uholanzi jana, kufuatia kutolewa na Ujerumani kwa kipigo cha mabao 7-1 katika Nusu Fainali.
    James Rodriguez wa Colombia amekuwa mfungaji bora kwa mabao yake sita, licha ya timu yake kutolewa Robo Fainali. Amefuatiwa na Thomas Muller wa Ujerumani mabao matano, Lionel Messi mabao manne sawa na Robin van Persie wa Uholanzi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MESSI MCHEZAJI BORA KOMBE LA DUNIA 2014, NEUER KIPA BORA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top