Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
TIMU ya Asswidiq imeifunga mabao 3-1 Twalipo katika mchezo wa ufunguzi wa michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 15 ya Rollingston, uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo wa Kundi A kwa U15, mabao ya washindi yalifungwa na Abdulkarim Abubakar dakika ya 18, Pazi Abdul dakika ya 21 na Hilal Fadhil dakika ya 39, wakati bao pekee la Twalipo lilifungwa na Bakari Omar dakika ya 55.
Mchezo wa pili wa kundi baina ya Kino na Bombom ulishindwa kufanyika kutokana na timu kutofika uwanjani.
Kwa miaka yote, michuano ya Rollingston imekuwa ikifanyika mjini Arusha pekee, lakini mwaka huu imebisha hodi hadi Dar es Salaam.

![]() |
| Wachezaji wa Asswidiq wakishangilia ushindi wao leo Chamazi |
Mchezo wa pili wa kundi baina ya Kino na Bombom ulishindwa kufanyika kutokana na timu kutofika uwanjani.
Kwa miaka yote, michuano ya Rollingston imekuwa ikifanyika mjini Arusha pekee, lakini mwaka huu imebisha hodi hadi Dar es Salaam.

.png)
0 comments:
Post a Comment