| Mshambuliaji mpya wa Yanga SC, Emmanuel Okwi pichani akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindo ya klabu hiyo, Mussa Katabaro, ameendelea kupiga danadana kuja kujiunga na wenzake kwa ajili ya mazoezi. Okwi pamoja na Mganda mwenzake, Hamisi Kiiza hawakufika jana Dar es Salaam kama walivyoahidi na sasa wameahidi kufika leo, lakini hadi sasa hawajafika. Picha ya chini ni Kiiza akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Abdallah Ahmwed Bin Kleb.
|
0 comments:
Post a Comment