• HABARI MPYA

    Wednesday, December 04, 2013

    YANGA INAJIENDESHA KWA HASARA TUPU, WAFADHILI WAKIBWAGA MANYANGA NI KIFO JANGWANI

    Na Mwandishi Wetu, Jangwani
    UONGOZI wa klabu ya Yanga leo umetoa ripoti ya mapato na matumizi kwa kipindi cha miezi sita tangu Januari 14, 2013 mpaka Julai 14, 2013 ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa kutoa mahesabu hayo kwa wapenzi, washabiki, na wanachama na jamii  kwa ujumla.
    Kwa mujibu wa tovuti ya klabu hiyo, baadhi ya gharama kubwa kwa klabu ni pamoja na usajili wachezaji na mishahara. Akizungumza na Waandishi wa habari juu ya mahesabu hayo katibu mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako amesema mapato makubwa ya klabu yanatokana na viingilio vya mechi na ufadhili.
    Mwenyekiti wa Yanga na mfadhili Mkuu wa klabu hiyo, Yussuf Manji

    Juhudi mbalilmbali zinafanyika kuongeza kipato cha klabu kama kuingia mikataba ya ufadhili, kutumia haki miliki za klabu.
    Uongozi unajitahid kuweza kudhibiti matumizi ya klabu kama njia moja ya kuhakikisha klabu inajitegemea.
    Klabu bado inaendelea kutegemea ufadhili wa TBL ambao kwa sasa inapata wastani wa mIL 30.25 kila mwezi, Madhumuni ya ufadhili huu ni kuwezesha klabu kulipia mishahara ambayo wastani inzaidi mil 60 kwa mwezi. Tayari klabu imeshaomba mazungumzo na mfadhili kuboresha mkataba huo.
    Katika kipindi cha Januari 2013 hadi Julai 2013 klabu iliweza kupata mil 110 kama zawadi mbalii mbali za ushindi ikiwemo mil 15 kutoka vodacom kwa kuwa timu yenye nidhamu.
    Bado kuna mali za klabu hazija thaminiwa zikiwemo majengo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA INAJIENDESHA KWA HASARA TUPU, WAFADHILI WAKIBWAGA MANYANGA NI KIFO JANGWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top