• HABARI MPYA

    Wednesday, December 04, 2013

    NGASSA KUNANI? MECHI TATU CHALLENGE HAKUNA BAO HATA LA OFFSIDE!

    MRISHO Khalfan Ngassa ‘Anko’ amekamilisha mechi tatu za makundi katika michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge bila kufunga bao ‘hata la offside’.
    Ngassa akiwa benchi leo Uwanja wa Afraha baada ya kutolewa

    Mshambuliaji huyo wa Yanga amecheza mechi ya tatu leo ya Kundi B na kutolewa dakika ya 81 akimpisha Ramadhani Singano ‘Messi’ akiwa hajapiga hata shuti moja langoni mwa Burundi, Stars ikishinda 1-0 zaidi ya mpira wa adhabu ambao haukuwa na madhara. Lakini Ngassa ndiye aliyetoa pasi ya bao la Stars leo lililofungwa na Mbwana Samatta dakika ya saba. 
    Hii ni mech ya pili mfululizo Ngassa anatolewa baada kutolewa pia katika mechi iliyopita dhidi ya Somalia, alipotolewa dakika 79 kumpisha Farid Mussa.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NGASSA KUNANI? MECHI TATU CHALLENGE HAKUNA BAO HATA LA OFFSIDE! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top