![]() |
| Dan Sserunkuma wa Uganda akimtoka beki wa Sudan, Malik Mohamed katika mchezo wa Kundi C leo Uwanja wa Nyayo. Uganda ilishinda 1-0. |
BAO pekee la kiungo Khalid Aucho dakika ya 47, limeipa Uganda ushindi wa 1-0 Uganda dhidi ya Sudan katika mchezo wa mwisho wa Kundi C, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge Uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya jioni hii.
ROBO FAINALI ZA CHALLENGE…
Desemba 7, 2013;
Uganda VS Tanzania
Kenya VS Rwanda
Desemba 8, 2013
Kenya VS Rwanda
Desemba 8, 2013
Zambia VS Burundi
Ethiopia VS Sudan
Ethiopia VS Sudan
Robo Fainali zitachezwa Uwanja wa Manispaa, Mombasa, Kenya Jumamosi na Jumapili
Mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Emmanuel Okwi alicheza tangu mwanzo, lakini nyota wa Yanga SC, Hamisi Kiiza aliingia kipindi cha pili, wakati Dani Sserunkuma wa Gor Mahia alicheza kipindi cha kwanza pekee.
Kocha wa zamani wa Yanga, Milutin Sredojevic ‘Micho’ alikuwa mwenye furaha baada ya mechi kwa sababu anakutana na Tanzania, ambayo aliifunga katika mechi za kufuzu za CHAN nyumbani na ugenini.
Baada ya matokeo ya leo, Uganda imeongoza Kundi C kwa pointi zake tisa na Sudan imekuwa ya pili kwa pointi zake sita. Uganda itacheza na Tanzania Bara katika Robo Fanali, wakati Kenya itacheza na Rwanda, Zambia na Burundi na Ethiopia na Sudan.
Mechi zote za Robo Fainali zitachezwa Uwanja wa Manispaa mjini Mombasa Jumamosi na Jumapili, wakati Nusu Fainali zitarudi Nyayo, ingawa iwapo uwekaji nyasi bandia katika Uwanja wa Moi, Kisumu utawahi kukamilika basi Nne Bora zitachezwa na huko, wakati fainali ni Nairobi.

| Beki wa Uganda, Mpuga Martin akiruka juu kupiga mpira kichwa dhidi ya mshambuliaji wa Sudan, Salah Ibrahim |
![]() |
| Dani Sserunkuma akimtoka Malik Mohamed |
![]() |
| Emmanuel Okwi akimfunga tela beki wa Sudan |

.png)
0 comments:
Post a Comment