• HABARI MPYA

    Friday, December 06, 2013

    SERIKALI KENYA YAIPA MZIGO FKF KUMALIZA ‘VIMEO’ CHALLENGE

    Na Mahmoud Zubeiry, Nairobi
    SERIKALI ya Kenya imelipa ahueni Shirikisho la Soka Kenya (FKF), wenyeji wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge Cup, kwa kutoa fedha za gharama za tiketi za ndege malazi kwa timu zote zilizopo katika mashindano hayo.
    Mwenyekiti wa FKF, Sam Nyamweya kushoto akiwa na Mwenyekiti wa CECAFA, Leodegar Tenga kulia

    “Hii ni kukujulisha kwamba tumepokea ombi kutoka FKF kuwasaidia kulipa bili zao. Tumekubaliana kuwalipia mara moja” imesema barua ya Waziri wa Michezo Sanaa na Utamaduni wa Kenya ya leo Desemba 6, iliyosainiwa na Katibu wa Wizara, Patrick Omutia.
    Serikali ya Kenya italipa shilingi 41,386,026 za Kenya, kati ya hizo Sh. 8,643,026 zikienda kwenye gharama za tiketi na zitakazobaki zitagharamia malazi katika hoteli sita West Breeze (1,836,000), Strand (3,672,000), Mvuli (2,808,000), Hill Park (14,145,600), Sandton (2,937,400) na Milele (7,344,000).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SERIKALI KENYA YAIPA MZIGO FKF KUMALIZA ‘VIMEO’ CHALLENGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top