• HABARI MPYA

    Saturday, December 07, 2013

    SALAMU ZAMIMINIKA KUITAKIA KILA LA HERI STARS MBELE YA UGANDA

    Na Zaituni Kibwana, Mombasa
    SALAMU za kuitakia heri timu ya soka ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars zimemiminika mjini Mombasa, ambako mchana huu timu hiyo itamenyana na mabingwa watetezi, Uganda The Cranes katika Robo Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge Uwanja wa Manispaa.
    Zacharia Hans Poppe ametuma saamu kutoka Lubumbashi na chini ni Wakili mpya, Evodius Mtawala naye pia ametuma salamu kutoka Dar es Salaam

    Wakala wa wachezaji anayetambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Yussuf Bakhresa ametuma ujumbe mfupi, ukisema; “Go Stars, go inshaallah,”, wakati Mwenyekiti wa kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema; “All the best Stars”.
    Mmiliki wa hoteli ya Sapphire Court, Abdulfatah Salum Saleh aliye ziarani Amerika, Ulaya na Asia ametuma ujumbe kutoka Italia akisema; “Mungu ibariki Tanzania, ibariki Stars” wakati Katibu wa Simba, Evodius Mtawala ambaye jana tu amebarikia na Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande kuwa Wakili amesema; “Kila la heri Stars, ushindi ni wetu,”.
    Yussuf Bakhresa ametuma salamu kutoka Dar es Salaam na chini na Abdulfatah Salim Saleh ametuma salamu kutoka Vatrican City, Italia 

    Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga SC, Mussa Katabro pia ameungana na Katibu wa Azam FC, Nassor Idrissa kuitakia kila heri Stars, wakituma ujumbe unaofanana; “Alle best Stars”.
    Watu wengi zaidi wametuma ujumbe BIN ZUBEIRY kuitakia ushindi Stars katika mchezo wake wa leo, ambao unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisima.    
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SALAMU ZAMIMINIKA KUITAKIA KILA LA HERI STARS MBELE YA UGANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top