• HABARI MPYA

    Saturday, December 07, 2013

    POULSEN APANGUA TENA KIKOSI STARS, HIMID NJE BEKI LA RUVU LINAANZA KULIA LEO, WENGINE WOTE WALE

    Na Mahmoud Zubeiry, Mombasa
    KOCHA Mdenmark, Kim Poulsen amefanya mabadiliko tena katika kikosi chake cha kwanza cha Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars akimuanzisha beki halisi, Michael Pius Aidan wa Ruvu Shooting, badala ya kiungo wa zam FC, Himid Mao Mkami ambaye amekuwa akimtumia katika beki ya kulia kwenye mechi zote za awali za Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge nchini hapa.
    Amepumzika kiasi cha kutosha; Michael Aidan ataanza beki ya kulia dhidi ya Uganda 
     

    Wakati Aidan atacheza kulia, Erasto Nyoni atacheza kushoto na katikati wataendelea kucheza Said Morad na Kevin Yondan, kiungo mkabaji Frank Domayo, mchezeshaji Salum Abubakar ‘Sure Boy’ wa pembeni, Mrisho Ngassa kulia na Amri Kiemba kushoto, wakati washambuliaji ni Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu.
    Kikosi cha Uganda ni; Benjamin Ochan, Nico Wadada, Muga Martin, Geoffrey Kizito, Godfrey Walusimbi, Kasaga Richard, Khalis Aucho, Mpande Joesph, Daniel Sserunkuma, Hamisi Kiiza na Emmanuel Okwi.  
    Mchezo wa Robo Fainali ya kwanza ya CECAFA Challenge unaanza saa nane kamili mchana huu Uwanja wa Manispaa, Mombasa, Kenya na utafuatiwa na mechi kati ya wenyeji Kenya na Rwanda.
    Robo Fainali nyingine ni kesho ni kati ya Ethiopia na Sudan na Burundi na Zambia Uwanja huo huo wa Manispaa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: POULSEN APANGUA TENA KIKOSI STARS, HIMID NJE BEKI LA RUVU LINAANZA KULIA LEO, WENGINE WOTE WALE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top