Na Mahmoud Zubeiry, Nakuru
MRISHO Khalfan Ngassa ‘Anko’ ni miongoni mwa wachezaji waliotarajiwa kung’ara
katika michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA
Challenge mwaka huu nchini Kenya, lakini hadi sasa hafajatisha.
Mshambuliaji huyo wa Yanga amecheza mechi mbili za makundi bila kufunga
hata bao moja na katika mechi dhidi ya Somalia alitolewa dakika 79 kumpisha
Farid Mussa.
![]() |
| Ngassa akienda benchi amechaka matope dhidi ya Somalia, lakini hakufunga bao |
Tayari washambuliaji wawili wa TP Mazembe, Mbwana Samatta na Thomas
Ulimwengu wamewasili Kenya kukiongezea nguvu kikosi cha Tanzania Bara,
Kilimanjaro Stars na bila shaka kocha Kim Poulsen atawaanzisha wote leo.
Na kama itakuwa hivyo, Ngassa atacheza pembeni katika mechi hiyo inayoanza
saa 8:00 mchana wa leo, hivyo kuwa na jukumu la kuwatengenezea nafasi zaidi
Samatta na Ulimwengu.
Lakini kwa kuwa Samatta na Ulimwengu nao wakati mwingine husogea pembeni,
Ngassa anaweza akawa na nafasi ya kufunga hata kwa kuingia moja kwa moja
kutokea pembeni.
Tayari mashabiki nchini Kenya wamekwishaanza kumpuuza Ngassa wakiamini
makali yake yameanza kupata kutu, lakini ukweli wa yote utajulikana leo baada
ya mechi na Burundi. Anko Ngassa aliyewakosa Somalia, atawapata Burundi
leo?



.png)
0 comments:
Post a Comment