• HABARI MPYA

  Saturday, October 21, 2017

  SUPERSPORT WAJIPA MOYO WATAWANG'OA CLUB AFRICAIN KWAO

  TIMU ya SuperSport United ya Afrika Kusini inaamini itaingia fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika licha ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Club Africain ya Tunisia kwenye mchezo wa kwanza nyumbani.
  SuperSport wamesafiri kuifuata Africain nchini Tunisia kwa mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali ya michuano hiyo, wakitoka kutoa sare ya 1-1 Oktoba 1 mjini Pretoria.
  Nahodha wa Matsantsantsa, Dean Furman, beki Grant Kekana na mshambuliaji Jeremy Brockie wamesema kwamba wameelekeza nguvu zao kwenye mchezo wa marudiano ili washinde na kwenda fainali ambako wako tayari kukutana na yeyote kati ya TP Mazembe ya DRC na FUS Rabat ya Morocco.
  Mazembe imetanguliza mguu mmoja fainali baada ya ushindi wa 1-0 Oktoba 1 kwenye mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali mjini Lubumbashi dhidi ya Rabat bao pekee la Ben Malango Ngita.
  FUS watajaribu kupindua matokeo katika mchezo wa marudiano na Mazembe kesho mjini Rabat ili kwenda fainali.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SUPERSPORT WAJIPA MOYO WATAWANG'OA CLUB AFRICAIN KWAO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top