• HABARI MPYA

  Saturday, October 21, 2017

  LIGI YA VIJANA AZAM YAENDELEA LEO MECHI TATU KUPIGWA COMPLEX

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  LIGI ya vijana chini ya umri wa miaka 15 ya Azam (Azam Youth League U-15) asubuhi ya leo inaingia katika wiki ya pili kwa mechi tatu kupigwa katika viunga vya Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Wenyeji Azam U-15 wanaongoza ligi hiyo baada ya kuanza kwa kishindo kwa kuifunga Florida 6-0 Jumamosi iliyopita, watakipiga dhidi ya Rendis saa 4.30 asubuhi.
  Rendis katika mchezo wake uliopita ilishinda 4-1 dhidi ya New Talent, ambayo imeondolewa kwenye michuano hiyo baada ya kushindwa kuthibitisha umri wa wachezaji wake na nafasi yake kuchukuliwa na Tanzanite ambayo inatokea Temeke, Dar es Salaam.
  Mechi nyingine leo, itashuhudiwa Tanzanite itakayocheza mechi yake ya kwanza baada ya kuchukua nafasi ya vijana wa Talents, ikikabiliana na JMK Park, ambayo kwenye mchezo wa kwanza iliilaza Bom Bom 4-2.
  Florida iliyotoka kupewa kipigo kizito dhidi ya Azam U-15, itashuka tena dimbani kujiuliza pale itakapochuana na Bom Bom ambayo nayo imetoka kupoteza mchezo wa kwanza, zote zikiburuza mkia kwenye ligi hiyo.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIGI YA VIJANA AZAM YAENDELEA LEO MECHI TATU KUPIGWA COMPLEX Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top