• HABARI MPYA

    Monday, October 16, 2017

    KATWILA: MTIBWA HATUKUZIBAHATISHA SIMBA NA YANGA, NI MIPANGO NA UWEZO

    Na Salma Suleiman, DAR ES SALAAM
    KOCHA wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila amesema kwamba hawajazibana Yanga na Simba Dar es Salaam kwa kubahatisha, bali ni sehemu ya mkakati wao wa kufanya vizuri katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu.
    Mtibwa Sugat ilitoa sare ya 1-1 na Simba SC jana wiki mbili tu baada ya kutoa sare ya 0-0 na Yanga, mechi zote zikipigwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
    Katika mchezo wa jana, Mtibwa walitangulia kwa kwa bao la Stahmili Mbonde dakika ya 35 kwa kichwa akiunganisha mpira wa kona uliopagwa na beki wa zamani wa Simba, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, kabla ya wenyeji kusawazisha kwa bao la mpira wa adhabu la Mganda, Emmanuel Okwi dakika ya 90 na ushei.
    Kocha wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila (kulia) akisalimiana na kocha wa Simba, Mcameroon Joseph Marius Omog

    Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online jana baada ya mchezo, Katwila alisema kwamba mchezo dhidi ya Simba ulikuwa mgumu, lakini waliingia na mkakati wa kupata bao la mapema ili kuwanyong’onyesha wapinzani wao. 
    “Katika mchezo huu tulikuja na lengo la kupata bao la mapema kutokana na kuwatambua wapinzani wetu na tunashukuru tulifanikiwa katika hilo, bahati mbaya wakati tunaamini tunashinda, wenzetu wakapata bao la kusawazisha, ila tunashukuru kupata pointi moja ugenini si jambo ndogo,” alisema.
    Katwila alisema anatambua timu kubwa za Simba na Yanga ukiingia kucheza nazo lazima uanze kwa tahadhari ya hali ya juu, ili kuepuka kuwapa nafasi ya kuanza kukufunga.
    Lakini Katwila pia akasema bao la kusawazisha la wapinzani wake, lilitaka kuwavuruga vijana wake kwa sababu lilikuja wakiwa wanaamini wamekwishashinda mechi.
    “Goli la Simba la kusawazisha lilifungwa katika wakati mbaya, wachezaji wangu walijua wamekwishashinda, kwani muda ulikwishaenda sana, hvyo imewaumiza sana na kusababisha wazozane wao kwa wao kutokana na kuonekama kama kuna mmoja alifanya makosa,” alisema.
    Katwila alisema kama kocha aliwatuliza vijana wake na kuwaambia mambo kama hayo hutokea katika michezo, hivyo wasahau yaliyopita na kuelekeza nguvu zao katika mchezo ujao dhidi ya Tanzania Prisons Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KATWILA: MTIBWA HATUKUZIBAHATISHA SIMBA NA YANGA, NI MIPANGO NA UWEZO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top