• HABARI MPYA

  Monday, April 03, 2023

  YANGA SC WAKABIDHIWA SH MILIONI ZA MAMÁ SAMIA BAO DHIDI YA MAZEMBE


  MSEMAJI Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa leo amewakabidhi Yanga SC Sh. Milioni 5 za zawadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan kwa bao lao walilofunga kwenye mechi dhidi ya TP Mazembe.
  Yanga walishinda 1-0 jana dhidi ya wenyeji, TP Mazembe Jijini Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) jana kwenye mchezo wa mwisho wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika.
  Rais Samia amekuwa akitoa Sh. Milioni 5 kwa kila bao la Yanga kwneye Kombe la Shirikisho na kiasi kama hicho pia kwa watani wao, Simba SC kwa kila bao wanalofunga kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kuanzia Hatua ya makundi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC WAKABIDHIWA SH MILIONI ZA MAMÁ SAMIA BAO DHIDI YA MAZEMBE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top