• HABARI MPYA

  Sunday, April 02, 2023

  WAZIRI DK. PINDI CHANA AHAMASISHA WATANZANIA KUSHIRIKI MCHEZO WA BAISKELI


  WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Dk. Pindi Chana ametoa Rai kwa Watanzania waendelee kujitokeza na  kushiriki mashindano ya mbio za Baiskeli yanayofanyika ndani na nje ya nchi.
  Balozi Dkt. Pindi Chana ametoa rai hiyo jana Aprili 01, 2023 jijini Dar es Salaam alipokutana na Mwendesha Baiskeli Bora Duniani, Mike Leszek Mikulski kutoka nchini Poland. Leszek amekuja nchini Tanzania kuweka rekodi ya kupanda Mlimani Kilimanjaro na kushuka kwa muda wa saa 24 zoezi atakalolifanya mwezi Septemba na Oktoba, 2023.
  "Natoa wito kwa Watanzania wanaopenda na kushiriki mchezo wa Baiskeli  wajisajili katika Chama Cha Baiskeli maana ni mchezo ambao una fursa mbalimbali, na sisi Serikali tumedhamiria kuunga mkono na kuitangaza nchi yetu kupitia Utamaduni, Sanaa na Michezo,” amesema Balozi Dkt. Pindi Chana.
  Kwa upande wake Leszek ameishukuru Serikali kwa kupata nafasi ya kufanya mchezo huo nchini Tanzania kupitia Taasisi yake ya "Unaweza Project" ambapo amesema lengo lake ni kufungua milango kwa Watanzania kupenda mchezo huo, kuongeza kujiamini na kusaidia nchi yao.
  Zaidi ya watu 200 wakiwemo Wanahabari wa Kimataifa na Kamati ya Dunia ya Guiness watashiriki kushuhudia rekodi hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WAZIRI DK. PINDI CHANA AHAMASISHA WATANZANIA KUSHIRIKI MCHEZO WA BAISKELI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top