• HABARI MPYA

    Tuesday, April 04, 2023

    UTAMADUNI NA MICHEZO KUZINGATIWA KATIKA DIRA YA MAENDELEO YA TAIFA 2050


    MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, amezindua Mchakato wa Maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050 leo Aprili 3, 2023 jijini Dodoma.
    Akizungumza katika tukio hilo, Makamu wa Rais Dkt. Mpango amesema mchakato huo lazima uzingatie fursa zilizopo katika Kubidhaisha Lugha ya Kiswahili, kukuza na kuendeleza Utamaduni, Mila na Desturi za Taifa pamoja na kukuza Sekta ya ubunifu, burudani na michezo.
    "Nitoe rai kwenu waandaaji wa Dira hii kuzingatia fursa zilizopo kwa vijana pamoja na kutumia fursa ambazo bado hatujazitumika pamoja na Sekta za Ubunifu (Creative Industry) .”Alisisitiza Dkt. Mpango.
    Hafla hiyo ya uzinduzi imehudhuriwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara, Nicholas Mkapa, viongozi wengine wa Serikali, Vyama vya siasa na Wananchi.
    Mchakato wa uandaaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050 inaandaliwa kutokana na kukamilika kwa Dira ya mwaka 2025 ambayo inakaribia kukamilika kwa mafanikio makubwa katika ukuaji wa uchumi na ustawi wa Taifa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UTAMADUNI NA MICHEZO KUZINGATIWA KATIKA DIRA YA MAENDELEO YA TAIFA 2050 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top