• HABARI MPYA

  Monday, April 03, 2023

  AZAM FC WAICHAPA MTIBWA 2-0, WATINGA NUSU FAINALI ASFC


  WENYEJI, Azam FC wamefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Mabao ya Azam FC yamefungwa na viungo washambuliaji, Muivory Coast, Kipre Junior dakika ya  27 na mzawa, Abdul Suleiman Sopu dakika ya 73.
  Sasa Azam FC itakutana na mshindi wa Robo Fainali ya tatu kati ya Simba SC na Ihefu katika Nusu Fainali.
  Singida Big Stars ilikuwa ya kwanza jana kutinga Ñusu Fainali baada ya ushindi wa 4-1 dhidi ya Mbeya City Uwanja wa LITI mjini Singida.
  Singida Big Stars watakutana na mshindi wa Robo Fainali ya mwisho baina ya Mabingwa watetezi, Yanga SC dhidi ya Ihefu SC katika Nusu Fainali.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC WAICHAPA MTIBWA 2-0, WATINGA NUSU FAINALI ASFC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top