• HABARI MPYA

    Wednesday, April 05, 2023

    SEKTA ZA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO KUENDELEA KUPEWA KIPAUMBELE MWAKA FEDHA 2023/24


    WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amewasilisha Hotuba ya Ofisi yake kwa mwaka 2023/24 Bungeni jijini Dodoma leo April 5, 2023, ambapo ameeleza kuwa Sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo zitaendelea kupewa kipaumbele katika kutekeleza majukumu yake.
    Katika hotuba hiyo, Mhe. Kassim Majaliwa amesema kuwa, katika mwaka wa fedha wa 2022/23, Lugha ya Kiswahili imeendelea kufanya vizuri Kimataifa ambapo takriban vituo 30 vya kufundisha Kiswahili kati ya hivyo 10 vipo  katika  Balozi ikiwemo Ufaransa,  Uholanzi,  Korea Kusini, Maritus, Nigeria, Sudan na Zimbabwe  na vituo  4 nje ya Balozi ambavyo ni Afrika Kusini, Italia, Ujerumani na Ethiopia.
    Ameongeza kuwa, Tanzania imeingia makubaliano na Nchi ya Afrika Kusini kutumia lugha ya Kiswahili kama lugha ya kujifunzia, ambapo pia ameeleza kuwa Kupitia Kituo Cha Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika kimeanzisha Utalii wa Kitamaduni katika Kituo hicho.
    Mhe. Majaliwa ameendelea kuongeza kuwa, Serikali imehusisha Mfuko wa Utamaduni na Sanaa ambapo hadi kufikia Februari 2023, takriban Shilingi Bilioni 1 imetumika kukopesha Wadau wa Sanaa ili kuendelea kutengeneza kazi bora zaidi.
    "Natumia nafasi hii kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza ari katika Sekta ya Michezo kwa kutoa hamasa ya kutoa zawadi ya  Shilingi Milioni 5 kwa kila Goli kwa Klabu za Simba na Yanga ambazo zinashiriki mashindano ya Afrika pamoja na ahadi ya Milioni 500  kwa Taifa Stars itakapofuzu AFCON mwaka 2024.
    Aidha, Mhe. Waziri Mkuu Majaliwa amesema mwaka ujao wa fedha 2023/24 Serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya michezo ikiwemo ujenzi wa Viwanja, Shule 56 za michezo, pamoja na kuendelea kubidhaisha lugha ya kiswahili, Kuendesha programu ya Mtaa kwa Mtaa hadi ngazi ya Taifa pamoja na mashindano ya michezo ya Taifa Cup.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SEKTA ZA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO KUENDELEA KUPEWA KIPAUMBELE MWAKA FEDHA 2023/24 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top