• HABARI MPYA

  Wednesday, April 05, 2023

  SIMBA SC YAANGUKIA KWA MABINGWA WATETEZI, WYDAD CASABLANCA


  TIMU ya Simba SC itamenyana na mabingwa watetezi, Wydad Casablanca ya Morocco katika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ikianzia nyumbani na kumalizia ugenini. 
  Robo Fainali nyingine za Ligi ya Mabingwa ni Al Ahly ya Misri na Raja Casablanca, CR Belouizdad ya Algeria dhidi ya Mamelodi Sundowns na JS Kabylie ya Algeria pia dhidi ya Espérance ya Tunisia/
  Mechi za kwanza zitachezwa kati ya Aprili 21 na 22 na marudiano kati ya Aprili 28 na 29.
  Mshindi kati ya Wydad na Simba atakutana na mshindi wa mchezo kati ya CR Belouizdad ya Algeria na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini 
  Simba imewahi kuwatoa mabingwa wa Afrika wa mwaka 2003, Zamalek kwa penalti baada ya kila timu kushinda 1-0 nyumbani kwake na mechi ya mwisho ilichezwa Cairo.
  RATIBA KAMILI ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA
  Simba SC   v    Wyedad Casablanca 
  Al Ahly        v    Raja Casablanca 
  Belouizdad  v    Mamelodi Sundowns
  JS Kabylie   v     Espérance 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAANGUKIA KWA MABINGWA WATETEZI, WYDAD CASABLANCA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top