• HABARI MPYA

  Wednesday, April 05, 2023

  MUDATHIR YAHYA ASHINDA BAO BORA LA MAKUNDI CAF


  KIUNGO wa Yanga SC, Mudathir Yahya Abbas ameshinda kinyanga’nyiro cha Bao Bora la hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kutokana na bao lake alilofunga kwenye mechi ya ushindi wa 3-1 dhidi ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Februari 19 Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Lilikuwa bao la pili katika mchezo huo alilofunga dakika ya 11 akimalizia pasi ya mfungaji wa bao la kwanza, mshambuliaji Kennedy Musonda, wakati bao la tatu la Yanga lilifungwa na kiungo Mkongo, Tuisila Kisinda dakika ya 90 na ushei.
  Muda amewashinda wachezaji wengine waliofunga dhidi ya timu za DRC pia, Aymen Mahious wa USM Alger kwa bao alilofunga dhidi ya St. Eloi Lupopo, Aubin Kramo Kouamé wa ASEC Mimosa ya Ivory Coast kwa bao alilofunga dhidi ya Diables Noirs pia na Paul Acquah wa Rivers United kwa bao alilowafunga DC Motema Pembe.
  Katika Hatua nyingine, nyota wa Al Ahly ya Misri, Mahmoud Kahraba ameshinda Bao Bora la Hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika kwa bao alilofunga dhidi ya Al Hilal kwenye mechi ya mwisho ya Kundi B.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MUDATHIR YAHYA ASHINDA BAO BORA LA MAKUNDI CAF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top