• HABARI MPYA

    Monday, April 03, 2023

    US MONASTIR YAIACHIA YANGA UONGOZI KUNDI D


    WENYEJI, US Monastirienne wamekamilisha mechi zao za Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya AS Réal Bamako ya Mali Uwanja wa Olympique Hammadi Agrebi mjini Radès, Tunis nchini Tunisia.
    Mabao ya Monastir yamefungwa na beki Mtunisia, Saleh Harabi dakika ya 35 na mshambuliaji Mualgeria, Abdelhakim Amokrane dakika ya 90 na ushei, wakati bao pekee la Real Bamako limefungwa na kiungo wa Mali, Makan Samabaly.
    Kwa matokeo hayo, Monastir inafikisha pointi 13, Sawa na Yanga ya Tanzania ilioongoza Kundi kwa wastani mzuri wa mabao.
    Timu nyingine zilizoongoza nakundi mbali na Yanga ni; Marumo Gallants ya Afrika Kusini (A), ASEC Mimosas ya Ivory Coast (B) na FAR Rabat ya Morocco C.
    Ziliomaliza nafasi ya pili mbali na Monastir ni USM Alger ya Algeria (A), Rivers United ya Nigeria (B) na Pyramids ya Misri (C).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: US MONASTIR YAIACHIA YANGA UONGOZI KUNDI D Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top