• HABARI MPYA

  Tuesday, April 11, 2023

  MKURUGENZI MAYAY ALIPOWAPOKEA MABINGWA WA AFRIKA FOUNTAIN GATE


  NAIBU Mkurugenzi wa Michezo, Ally Mayay Tembele akipokea Kombe kutoka kwa Nahodha wa shule ya sekondari ya Fountain Gate ya Dodoma timu hiyo ilipowasili usiku huu Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam kutoka Afrika Kusini.
  Ijumaa Fountain Gate ilitwaa ubingwa wa michuano ya shule za sekondari Afrika kwa wasichana baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Ecole Omar IBN Khatab ya Morocco Uwanja wa King Zwelithini Jijini Durban, Afrika Kusini.
  Katika michuano hiyo iliyoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), mabao ya Fountain Gate yalifungwa na Winfrida Hubert mawili na Irene Chitanda moja na huo ulikuwa mchezo wa pili jana baada awali kuitandika SCG De Mfilou ya Kongo mabao 4-0 katika Nusu Fainali.
  Fountain Gate pia imetoa Mchezaji Bora wa Mashindano, Wilifrida Gerald ambaye pia ameibuka Mfungaji Bora kwa mabao yake 11, na Kipa Bora, Allic Neckema.
  Kwa kutwaa ubingwa huo, Fountain Fate imezawadiwa dola za Kimarekani 300,000, kiasi ambacho pia amepewa bingwa wa upande wa wavulana, huku washindi wa pili wakiondoka na dola 200,000 na wa tatu dola 150,000.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MKURUGENZI MAYAY ALIPOWAPOKEA MABINGWA WA AFRIKA FOUNTAIN GATE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top