• HABARI MPYA

  Saturday, April 08, 2023

  MAN UNITED YAICHAPA EVERTON 2-0 OLD TRAFFORD


  MABAO ya Scott McTominay dakika ya 36 na Anthony Martial dakika ya 71 yameipa Manchester United ushindi wa 2-0 dhidi ya Everton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
  Pamoja na ushindi huo, kocha Mholanzi wa Man United, Erik ten Hag alisikitishwa na kitendo cha mshambuliaji wake tegemeo, Marcus Rashford kushindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumia nyonga kipindi cha pili na nafasi yake kuchukuliwa na Wout Weghorst dakika ya 81.
  Kwa ushindi wa leo, Manchester United inafikisha pointi 56, ingawa inabaki nafasi ya nne ikizidiwa tu wastani wa mabao na Newcastle United baada ya wote kucheza mechi 29, wakati Everton inabaki na pointi zake 27 za mechi 30 nafasi ya 17.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAICHAPA EVERTON 2-0 OLD TRAFFORD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top