• HABARI MPYA

  Saturday, April 08, 2023

  FRANK LAMPARD AKARIBISHWA NA KICHAPO CHELSEA


  BAO pekee la Matheus Nunes dakika ya 31 leo limeipa Wolverhampton Wanderers FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Chelsea katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Molineux mjini Wolverhampton, West Midlands.
  Ulikuwa mchezo wa kocha Frank Lampard baada ya kurejea Chelsea kufuatia kufukuzwa kwa Graham Potter Jumapili iliyopita na kwa ushindi huo, Wolves wanafikisha pointi 31 na kusogea nafasi ya 12 wakizidiwa pointi nane na The Blues walio juu yao baada ya wote kucheza mechi 30.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FRANK LAMPARD AKARIBISHWA NA KICHAPO CHELSEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top