• HABARI MPYA

  Friday, April 07, 2023

  SINGIDA BIG STARS YAIBAMIZA POLISI TZ 3-0 LITI


  TIMU ya Singida Big Stars imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa LITI mjini Singida.
  Mabao ya Singida Big Stars leo yamefungwa na mabeki Pascal Wawa dakika ya 13, Nickson Kibabage dakika ya 57 na mshambuliaji Amissi Tambwe dakika ya 90.
  Kwa ushindi huo, Singida Big Stars inafikisha pointi 51 katika mchezo wa 26, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikiizidi pointi nne Azam FC ambayo usiku wa leo inacheza na Mtibwa Sugar.
  Hali inazidi kuwa mbaya kwa Polisi baada ya kichapo cha leo, kwani inaendelea kushika mkia ikibaki na pointi 19 za mechi 26 sasa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SINGIDA BIG STARS YAIBAMIZA POLISI TZ 3-0 LITI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top