• HABARI MPYA

  Monday, October 03, 2022

  COASTAL UNION YAICHAPA KAGERA SUGAR 2-0 MKWAKWANI


  WENYEJI, Coastal Union wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
  Mabao ya Coastal Union yamefungwa na Mbaraka Hamza yote, la kwanza kwa penalti dakika ya 10 na lingine dakika ya 65 na kwa ushindi huo, Wagosi wa Kaya wanafikisha pointi saba katika mchezo wa sita na kusogea nafasi ya tisa.
  Kwa upande wao, Kagera Sugar baada ya kichapo cha leo wanabaki na pointi zao mbili katika nafasi ya 15 baada ya kucheza mechi tano hadi sasa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: COASTAL UNION YAICHAPA KAGERA SUGAR 2-0 MKWAKWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top