• HABARI MPYA

  Wednesday, October 05, 2022

  MANE APIGA BONGE LA BAO BAYERN YASHINDA 5-0


  MSHAMBULIAJI Msenegal, Sadio Mane amewaonyesha mashabiki wa Liverpool wanachokikosa kwake baada ya kuifungia bao zuri timu yake mpya, Bayern Munich ikiibuka na ushindi wa 5-0 dhidi ya Viktoria Plzen katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
  Katika mchezo huo wa Kundi C uliofanyika Uwanja wa Allianz Arena Jijini Münich, Mane alifunga bao hilo dakika ya 21, wakati mabao mengine ya Bayern Munich yamefungwa na Leroy Sane mawili dakika ya saba na 50, Serge Gnabry dakika ya 13 na 
  Eric Choupo-Moting dakika ya 59.
  Bayern Munich inafikisha pointi tisa na kuendelea kuongoza kundi hilo kwa pointi tatu zaidi ya Inter Milan baada ya wote kucheza mechi tatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MANE APIGA BONGE LA BAO BAYERN YASHINDA 5-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top