• HABARI MPYA

  Tuesday, October 04, 2022

  IHEFU YAVUNA POINTI YA KWANZA MECHI YA TANO LIGI KUU


  WENYEJI, wamelazimishwa sare ya 1-1 na Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Highland Estate, Ubaruku, Mbarali mkoani Mbeya. 
  Ihefu walitangulia na bao la mshambuliaji Jaffary Kibaya dakika ya 55, kabla ya mtokea benchi Ismail Mgunda kuisawazishia Prisons dakika ya 81.
  Kwa matokeo hayo Ihefu inayookota pointi ya kwanza msimu huu katika mchezo wa tano, inaendelea kushika mkia, wakati Prisons inafikisha pointi nane katika mchezo wa sita nafasi ya nane.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: IHEFU YAVUNA POINTI YA KWANZA MECHI YA TANO LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top