• HABARI MPYA

  Tuesday, October 04, 2022

  GEITA GOLD YAPATA USHINDI WA KWANZA MSIMU HUU


  TIMU ya Geita Gold FC imepata ushindi wa kwanza wa msimu baada ya kuichapa Polisi Tanzania mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara mchana wa leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
  Mabao ya Geita Gold yamefungwa na George Mpole dakika ya 45 na Edmund John dakika ya 82, wakati bao pekee la Polisi Tanzania limefungwa na Hassan Kapona dakika ya 66.
  Kwa ushindi huo, Geita Gold inafikisha pointi sita katika mchezo wa sita na kusogea nafasi ya 12, wakati Polisi inabaki na pointi zake nne za mechi tano sasa nafasi ya 14.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GEITA GOLD YAPATA USHINDI WA KWANZA MSIMU HUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top