• HABARI MPYA

  Friday, July 02, 2021

  HISPANIA YAITOA USWISI KWA MATUTA, YATINGA NUSU FAINALI EURO 2020

  HISPANIA imetinga Nusu Fainali ya Euro 2020 baada ya ushindi wa penalti 3-1 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 120 leo Uwanja wa Saint-Petersburg Jijini Saint-Petersburg nchini Urusi.
  Mchezaji wa Borussia Monchengladbach, Denis Lemi Zakaria alianza kujifunga dakika ya  nane kuipatia Hispania bao la kuongoza, lakini kiungo mwenzake, Xherdan Shaqiri wa Liverpool kuisawazishia Uswisi dakika ya 68.
  Na kwenye mikwaju ya penalti Daniel Olmo, Gerard Moreno na Mikel Oyarzabal waliifungia Hispania huku Sergio Busquets na Rodri wakikosa na Mario Gavranović pekee akaifungia Uswisi kabla ya wenzake watatu kukosa.


  Hispania sasa itakutana na mshindi kati ya Italia na Ubelgiji katika Nusu Fainali Jumanne.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HISPANIA YAITOA USWISI KWA MATUTA, YATINGA NUSU FAINALI EURO 2020 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top