• HABARI MPYA

  Monday, January 04, 2021

  RONALDO AWAPIKU MESSI NA PELE KWA REKODI YA KUFUNGA MABAO


  MSHAMBULIAJI Cristiano Ronaldo jana amefunga mabao mawili kuiwezesha Juventus kupata ushindi wa 4-1 dhidi ya Udinese katika mchezo wa Serie A Uwanja wa Allianz mjini Torino na sasa ni wa pili  kwa kufunga mabao mengi kihistoria kwenye ngazi ya klabu na nchi akimpiku gwiji wa Brazil, Pele na sasa anahitaji bao moja zaidi kufikia rekodi ya Josef Bican.
  Ronaldo mwenye umri wa miaka 35 jana amefunga bao la 757 na 758 na sasa ana wastani wa kufunga mabao 42 kwa msimu kwenye klabu na nchi, akimzidi Pele mwenye mabao 757, wote wakiwa nyuma ya Josef Bican mwenye mabao 759.
  Lionel Messi anamfuatia Ronaldo kwenye orodha akiwa na mabao 742, lakini amecheza mechi chache, 200 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RONALDO AWAPIKU MESSI NA PELE KWA REKODI YA KUFUNGA MABAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top