• HABARI MPYA

  Monday, January 04, 2021

  MAN CITY YAIFUMUA CHELSEA 3-1 PALE PALE STAMFORD BRIDGE


  Manchester City imeibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Chelsea jana katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
  Mabao ya Manchestr City yalifungwa na viungo Ilkay Gundogan dakika ya 18, Phil Foden dakika ya 21 na mshambuliaji Kevin de Bruyne dakika ya 34, wakati bao pekee la Chelsea lilifungwa na Callum Hudson-Odoi dakika ya 90 na ushei.
  Manchester City inafikisha pointi 29 baada ya kucheza mechi 15 na inasogea nafasi ya tano ikizidiwa wastano wa mabao tu na Tottenham Hotspur ambayo hata hivyo imecheza mechi moja zaidi, wakati  Chelsea inayobaki na pointi zake 26 za mechi 17 ni ya nane sasa 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY YAIFUMUA CHELSEA 3-1 PALE PALE STAMFORD BRIDGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top