• HABARI MPYA

  Jumapili, Agosti 26, 2018

  MTIBWA WAWAZIMA PRISONS 1-0 MANUNGU, MBAO FC WAIPIGA STAND UNITED 2-1 KAMBARAGE…JKT, RUVU SHOOTING WAJIKONGOJA!

  Na Mwandishi Wetu, MOROGORO
  TIMU ya Mtibwa Sugar leo imepata ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa bao 1-0 Tanzania Prisons katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji Stahmil Mbonde aliyefunga dakika ya 37 akimalizia pasi ya Riffat Hamisi.
  Hicho kinakuwa kipigo cha pili mfululizo katika mechi zote za ugenini kwa Tanzania Prisons, baada ya awali kufungwa pia 1-0 na Simba SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Mtibwa Sugar wanapata ushindi wa kwanza, baada ya kufungwa 2-1 na Yanga SC katika mchezo wa kwanza ugenini nao, Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  Mshambuliaji Stahmil Mbonde (kulia) akishangilia baada ya kufunga bao pekee leo 

  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Mbao FC wameendeleza wimbi la ushindi baada ya kuwafunga wenyeji, Tanzania Prisons 2-1 Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
  Iliwabidi Mbao FC kutoka nyuma kwa bao la Sixtus Sabilo dakika ya 31 na kuibuka kifua mbele kwa mabao ya Said Khamis dakika ya 57 na Pastory Athanas dakika ya 59.
  JKT Tanzania wamelazimishwa sare ya pili mfululizo nyumbani Uwanja wa Meja Isamuhuyo huko Mbweni, wakifungana 1-1 na Lipuli FC ya Iringa. Lipuli iliyotoa sare nyingine ugenini 1-1 na Coastal Union mjini Tanga katikati ya wiki ilitangulia kwa bao la Paul Nonga dakika ya 49, kabla ya Ally Bilal kuisawazishia JKT iliyotoka sare ya 0-0 na KMC katika mchezo wake wa kwanza dakika ya 75. 
  Ligi Kuu itaendelea kesho kwa michezo miwili, Simba SC wakiikaribisha Mbeya City Uwanja wa Taifa na Azam FC wakiwa wenyeji wa Ndanda FC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MTIBWA WAWAZIMA PRISONS 1-0 MANUNGU, MBAO FC WAIPIGA STAND UNITED 2-1 KAMBARAGE…JKT, RUVU SHOOTING WAJIKONGOJA! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top