• HABARI MPYA

  Ijumaa, Agosti 24, 2018

  KESI YA AKINA MALINZI YAAHIRISHWA TENA BAADA YA MAHAKAMA KUPOKEA NYARAKA YA KANUNI ZA FEDHA ZA TFF

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KESI inayowakabili waliokuwa viongozi wakuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Rais Jamal Malinzi na Katibu Mkuu, Selestine Mwesigwa imeahirishwa hadi Septemba 4, mwaka huu baada ya upande wa mashitaka kuwasilisha nyaraka ya kanuni za Fedha za shirikisho hilo.
  Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu mjini Dar es Salaam, Wilbard Mashauri mapema leo amepokea nyaraka ya kanuni za Fedha za TFF zilizowasilishwa na Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, Wilfred Kidau (41) .
  Mahakamani imepokea nyaraka hizo baada ya ombi la Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Leonard Swai.
  Mbali na Malinzi na Mwesigwa, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa Mhasibu wa TFF,  Nsiande Isawayo Mwanga, Meneja wa  Ofisi ya Shirikisho hilo, Miriam Zayumba na Karani, Flora Rauya.
  Aliyekuwa Rais wa TFF, Jamal Malinzi akisindikizwa na askari Magereza kutoka mahakamani leo kurejea gereza la Keko, Dar es Salaam

  Wakili Swai alidai kuwa kanuni za fedha za TFF za mwaka 2013 zilizofanyiwa marekebisho mwaka 2015 ilizopo kwenye sheria za Shirikisho hilo, zinatoa mwongozo wa kukopa fedha, hivyo kuiomba mahakamani ipokee nyaraka hizo na kuiongeza kwenye vielelezo vya ushahidi wa kesi hiyo.
  Lakini mawakili wa utetezi, Richard Rweyongeza na Abraham Senguji walipinga kupokelewa kwa nyaraka hiyo wakidai kwamba hizo ni nakala na siyo nyaraka halisi na kwamba imekuwa kama ya kutengeneza, jambo ambalo lilipingwa vikali na Wakili Swai. 
  Aidha, Wakili Swai alidai mahakamani hapo kwamba shahidi Kidau ambaye alitarajiwa kufika leo amepata udhuru wa ugeni kutoka Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFAHakimu Mashauri alipokea nyaraka hizo na kudai siyo sahihi kusema zimetengenezwa, kabla ya kuiahirisha kesi hiyo hadi Septemba 4, mwaka huu 2018 kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa shahidi wa upande wa mashtaka.
  Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 30 yakiwamo ya kughushi, kuwasilisha nyaraka za kughushi na utakatishaji fedha.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KESI YA AKINA MALINZI YAAHIRISHWA TENA BAADA YA MAHAKAMA KUPOKEA NYARAKA YA KANUNI ZA FEDHA ZA TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top