• HABARI MPYA

  Jumanne, Agosti 21, 2018

  FIFA YAINGILIA KATI SUALA LA CHAMA WA SIMBA…WAITAKA ZAMBIA KUTUMA ITC YAKE HARAKA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Simba imesema kwamba ina nafasi ndogo ya kuwatumia wachezaji wake wawili, kipa Deo Munishi ‘Dida’ na kiungo Mzambia, Cletus Chama katika mchezo wa kesho wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Tanzania Prisons Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  Msemaji wa klabu ya Simba, Hajji Sunday Manara amesema kwamba hiyo inatokana na wachezaji wote wawili kuwa bado hawajatumiwa Hati yake ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kutoka nchi walizokuwa wanacheza.
  Dida amejiunga tena na Simba SC mwezi uliopita akitokea timu ya Chuo Kikuu cha Pretoria nchini Afrika Kusini, wakati Chama amesajiliwa Julai pia kutoka Dynamos ya kwao.
  Cletus Chama yuko shakani kuichezea Simba SC dhidi ya Tanzania Bara kesho

  “Cletus Chama na Dida, ITC zao zimechelewa, lakini FIFA wamewaandikia barua Chama cha Mpira cha Zambia kuwapa muda hadi kesho wawe wametuma ITC ya Chama, kwa hiyo tunatarajia chama cha mpira cha Zambia kitatuma ITC hiyo kwa TFF ili tuweze kumtumia kiungo wetu bora kabisa, Cletus Chama,”amesema Manara.
  Dida na Chama mwenye umri wa miaka 27 aliyewahi kuchezea pia Ittehad ya Misri, ZESCO United FC na Nchanga Rangers FC, zote za kwao pia, Zambia hakucheza mechi ya Ngao ya Jamii Jumamosi SImba ikiichapa 2-1 Mtibwa Sugar kwa sababu ya ITC.
  Chama ni miongoni wachezaji nane wa kigeni, Simba SC baada ya mabeki Muivory Coast, Serge Wawa,  Pascal na mshambuliaji Mnyarwanda mwenye asili ya Uganda, Meddie Kagere, Waghana, beki Asante Kwasi, kiungo James Kotei na mshambuliaji Nicholas Gyan, Mganda Emmanuel Okwi na Mnyarwanda Haruna Niyonzima.
  Ligi Kuu inatarajiwa kesho na Wekundu wa Msimbazi, Simba SC watafungua dimba na Tanzania Prisons Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
  Na Simba SC itaingia kwenye mchezo huo ikitoka kushinda Ngao ya Jamii baada ya kuichapa Mtibwa Sugar mabao 2-1 Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: FIFA YAINGILIA KATI SUALA LA CHAMA WA SIMBA…WAITAKA ZAMBIA KUTUMA ITC YAKE HARAKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top