• HABARI MPYA

  Jumanne, Agosti 28, 2018

  MTOTO WA SIMEONE AIFUNGIA BAO FIORENTINA MBELE YA BABA YAKE

  CHIPUKIZI Giovanni Simeone aliifunga bao dakika ya 93 Fiorentina Jumapili na kwenda kumnyooshea mikono kishujaa baba yake, Diego aliyekuwa jukwaani.
  The Viola walianza michuano ya Ligi Kuu Italia, maarufu kama Serie A kwa ushindi wa 6-1 dhidi ya Chievo Jumapili, Simeone akifurahia burudani nzuri.
  Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka alipokea pasi kwenye boksi kabla ya kumtungua kipa wa Chievo. 
  Baada ya refa kupuliza filimbi ya kuhitimisha mchezo, kocha wa Fiorentina, Stefano Pioli alikwenda uwanjani kunyoosha mkono kumuonyesha kocha wa Atletico Madrid, Simeone.
  Giovanni Simeone akimnyooshea mikono baba yake kishujaa baada ya bao lake la dakika ya 93 dhidi ya Chievo

  Mshambuliaji huyo alifurahi kisha akatabasamu na kumnyooshea mikono kishujaa baba yake huyo maarufu. 
  Baba yake alionekana mwenye furaha kubwa na kupunga mikono mbele ya kamera akiwa na mkewe, Carla Pereyra na binti yao wa miaka miwili, Francesca.
  Diego Simeone ni mwanasoka mstaafu wa Argentina na klabu Vélez Sársfield, Pisa, Sevilla, Atlético Madrid, Inter Milan, Lazio, Atlético Madrid na Racing Club ambazo kwa pamoja alizichezea mechi 513 na kuzifungia mabao 84.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MTOTO WA SIMEONE AIFUNGIA BAO FIORENTINA MBELE YA BABA YAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top