• HABARI MPYA

  Jumatatu, Agosti 27, 2018

  MWINGINE TFF AFUNGIWA MAISHA KUJIHUSISHA NA SOKA KWA WIZI, KUGHUSHI NA UBADHIRIFU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KAMATI ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemfungia kutojishughulisha na mchezo huo maisha aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya shirikisho hilo na msimamizi wa kituo cha Shinyanga, Mbasha Matutu kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake.
  Taarifa ya TFF iliyotolewa leo imesema kwamba Matutu amefungiwa baada ya kikao cha Kamati ya Maadili kilichofanyika Jumamosi ya Agosti 25, mwaka huu makao makuu ya shirikisho hilo, Uwanja wa Karume mjini Dar es Salaam.

  Mbasha Matutu amefungiwa maisha kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake

  Na hiyo ni baada ya kukutwa na hatua ya makosa matatu ambayo ni ubadhirifu, kughushi na kuiba mambo ambayo ni kinyume na Kanuni za Maadili za TFF na Ligi Kuu.
  Matutu anakuwa kiongozi wa pili kufungiwa maisha ndani ya mwaka mmoja, baada ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa TFF, Michael Wambura na wote kwa makosa yanayoshabihiana.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MWINGINE TFF AFUNGIWA MAISHA KUJIHUSISHA NA SOKA KWA WIZI, KUGHUSHI NA UBADHIRIFU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top