• HABARI MPYA

  Ijumaa, Agosti 31, 2018

  CHELSEA NA LIVERPOOL KUKUTANA RAUNDI YA TATU CARABAO CUP


  Liverpool na Chelsea zitamenyana katika Raundi ya Tatu ya Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup 

  RATIBA RAUNDI YA TATU CARABAO CUP

  West Brom v Crystal Palace
  Arsenal v Brentford
  Burton v Burnley
  Wycombe v Norwich
  Oxford United v Manchester City
  West Ham v Macclesfield
  Millwall v Fulham
  Liverpool v Chelsea
  Bournemouth v Blackburn
  Preston v Middlesbrough
  Wolves v Leicester
  Tottenham v Watford
  Blackpool v QPR
  Everton v Southampton
  Manchester United v Derby
  Nottingham Forest v Stoke
  KLABU ya Liverpool imepangiwa kucheza na Chelsea katika Raundi ya Tatu ya Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup. 
  Wakati huo huo, Frank Lampard na timu yake ya Derby watamenyana na kocha wake wa zamani, Jose Mourinho wa Manchester United, baada ya wawili kufanya kazi kwa mafanikio makubwa wakiwa Chelsea, ikiwemo ushindi wa taji la Kombe la Ligi mwaka 2005.
  Mechi ya Liverpool dhidi ya Chelsea itakuja siku kadhaa kabla hawajamenyana wao kwa wao kwenye Ligi Kuu ya England Uwanja wa Stamford Bridge Septemba 29. 
  Wekundu hao wameuanza msimu huu katika kiwango kizuri, wakishinda mechi zao tatu mfululizo za mwazo na mchezo utakuwa wa kwanza kumkutanisha Jurgen Klopp na Maurizio Sarri England. 
  Chelsea iliifunga Liverpool kwenye Nusu Fainali ya Kombe la mwaka 2015.  
  Lampard alikuwa mmoja wa nyota waliombeba Jose Mourinho katika mafanikio yake alipokuwa Chelsea na walishinda mataji mawili ya Ligi Kuu.
  Lakini Mourinho yupo katika wakati mgumu United baada ya kuanza vibaya msimu, akifungwa mechi mbili kati ya tatu za Ligi Kuu. 
  Mabingwa watetezi, Manchester Citywatamenyana na timu ya Daraja la Kwanza, Oxford United, wakati Tottenham itawafuata Watford nyumbani kwao. Arsenal, waliofika fainali msimu uliopita watamenyana na timu ya Championship, Brentford.
  Timu ya Ligi Daraja la Pili, Macclesfield, ambayo ni ya kiwango cha chini zaidi katika mashindano, itamenyana na West Ham ugenini. Everton watacheza na Southampton na Wolveswatakuwa wenyeji wa Leicester katika mchezo wa timu za Ligi Kuu tupu. 
  Burnley, ambayo inaanzia hatua hii kwenye mashindano haya, watamenyana na timu ya Daraja la Kwanza, Burton ugenini wakati Crystal Palace watasafiri kuwafuata West Bromwich Albion.
  AFC Bournemouth pia wamepewa timu ya Championship, Blackburn Rovers ambao ndiyo watamenyana nao.
  Mechi hizo zitachezwa wiki inayoanzia Septemba 24. 


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHELSEA NA LIVERPOOL KUKUTANA RAUNDI YA TATU CARABAO CUP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top