• HABARI MPYA

  Jumatano, Agosti 22, 2018

  SHABIKI AJISHINDIA SH. MILIONI 1.7 ZA SPORTPESA KWA KUTABIRI KWA USAHIHI MATOKEO YA MECHI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SHABIKI wa soka, Enock Severin wa Masasi mkoani Mtwara amefanikiwa kujishindia jumla ya Sh 1, 746,331 kwa kutabiri kwa usahihi matokeo mechi nyingi kwa mtaji wa Sh 1, 000 tu kupitia kampuni ya SportPesa. 
  Severin alitabiri kwa usahihi matokeo ya michezo 20, huku mwenyewe akikiri kuwa hiyo ni mara yake ya kwanza kubashiri idadi kubwa ya michezo na kushinda. 
  "Nilibashiri jumla ya michezo ishirini na hii ni mara yangu ya kwanza kubashiri michezo mingi na mara baada ya mchezo wa mwisho nilitumiwa fedha zangu" alisema. 
  "Kwanza sikuamini, lakini nilipoona mchezo wa mwisho nilioubashiria umekamilika nikatumiwa fedha zangu, nawapongeza sana SportPesa" Aliongeza.

  Enock Severin wa Masasi amejishindia Sh Milioni 1.7 kwa kutabiri kwa usahihi matokeo mechi  

  Enock Severin ni mmoja kati ya maelfu wa watu wanaofaidika na alama (odds) bora na za kipekee zitolewazo na Sportpesa ukilinganisha na makampuni mengine ya ubashiri.
  Severin amethibitisha pia kwamba SportPesa wanaposema unabashiri na ukishinda hakuna ubabaishaji wa malipo ni sahihi na watumiaji wake kama ndugu Severin ni mashuhuda wa hilo. 
  Pamoja na kubashiri kawaida pia SportPesa wana Jackpot maalumu ambayo kwa kila atakayebahatika kubashiri michezo 13 kwa usahihi atafaidika na kiasi cha zaidi ya Sh. Milioni 310, lakini pia wachezaji wa Jackpot hiyo wanaopata kuanzia timu 10, 11 na 12 hufaidika kwa bonus.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SHABIKI AJISHINDIA SH. MILIONI 1.7 ZA SPORTPESA KWA KUTABIRI KWA USAHIHI MATOKEO YA MECHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top