• HABARI MPYA

  Jumatano, Agosti 29, 2018

  BERAHINO AMALIZA UKAME WA MABAO WA SIKU 913

  Mshambuliaji mzaliwa wa Burundi, Saido Berahino (katikati) akipongezwa na wenzake usiku wa jana baada ya kuifungia Stoke City bao la kwanza dakika ya 53 katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Huddersfield kwenye mchezo wa Raundi ya Pili ya Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup Uwanja wa Bet365 mjini Stoke-on-Trent, Staffordshire. Bao la pili Juninho Bacuna wa Huddersfield alijifunga dakika ya 90 na ushei.
  Mara ya mwisho Berahino alifunga akiwa West Bromwich Albion Februari mwaka 2016, yaani zimepita siku 913 na mechi 47, wakati huo Donald Trump alikuwa bado nyota wa TV. Johan Cruyff, George Michael, Prince, na Muhammad Ali wote walikuwa hai 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BERAHINO AMALIZA UKAME WA MABAO WA SIKU 913 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top