• HABARI MPYA

  Jumatano, Agosti 29, 2018

  ETO'O KUMJENGEA NYUMBA GWIJI WA CAMEROON OWONA

  GWIJI wa Cameroon, Samuel Eto’o amemchangia fedha Norbert Owona, Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya nchi hiyo, Simba Wasiofungika ambaye amekuwa hana makazi na mgonjwa.
  Kwa mujibu wa taarifa kadhaa, Owona akiishi ovyo mitaani tangu amepoteza familia yake kwa ajali. Amefilisika, amekuwa mgonjwa na hatimaye kupoteza makazi.
  Na baada ya hali kuwa ngumu kiasi cha kutokuwa na makazi, Owona akalazimika kuomba msaada.
  Na katika safari yake ya hivi karibuni nchini Cameroon, Eto’o akamtembelea gwiji mwenzake huyo aliyecheza nafasi ya kiungo miaka ya 1960 hadi 1970.

  Samuel Eto’o (kushoto) akiwa na Norbert Owona baada ya kumtembelea na kumpa matumaini mapya ya maisha  

  Taarifa kadhaa kutoka nchini Cameroon zinasema kwamba nyota huyo wa zamani wa Barcelona alimchangia faranga za Cameroon 500,000 Owona na kuahidi kumpa nyumba mpya ya kuishi.
  Owona aliichezea kwa miaka kadhaa timu ya taifa ya Cameroon na aliiwakilisha kwenye Fainali mbili za kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ETO'O KUMJENGEA NYUMBA GWIJI WA CAMEROON OWONA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top