• HABARI MPYA

  Alhamisi, Agosti 30, 2018

  TIMU YA BANDA YAVUNA POINTI TANO KATIKA MECHI TANO ZA MWANZO LIGI KUU YA AFRIKA KUSINI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BEKI wa kimataifa wa Tanzania, Abdi Banda na wachezaji wenzake wa Baroka FC wana kazi ya kufanya, kwani hadi sasa mwenendo wa timu yao si mzuri katika Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini kufuatia jana kulazimishwa sare ya 1-1 na Highlands Park Uwanja wa Peter Mokaba mjini Pietersburg.
  Wageni, Highlands Park walitangulia kwa bao la Thabo Motlafi aliyefunga dakika ya 75, zikiwa ni dakika 10 tu tangu aingie uwanjani kwenda kuchukua nafasi ya Petrus Ngebo, kabla ya Ranga Chivaviro kuisawazishia Baroka FC dakika ya 90.
  Sare hiyo ya pili ndani ya mechi tano, nyingine mbili ikifungwa na kushinda moja inaifanya Baroka FC ikusanye pointi tano ambao si wastani mzuri.

  Abdi Banda ana kazi ya kufanya kuisaidia Baroka FC, kwani mwenendo wake si mzuri katika Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini  

  Msimu uliopita, Baroka FC ilinusuruka kushuka Daraja baada ya kuchapwa bao 1-0 na SuperSport United katika mchezo wake wa mwisho wa Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini  Uwanja wa Lucas Masterpieces Moripe mjini Pretoria.
  Matokeo hayo yaliifanya SuperSport ifikishe pointi 36 baada ya kucheza mechi zote 30 za PSL msimu huu na kupanda hadi nafasi ya 11 kutoka ya 13, huku Baroka sasa ikiwa ya mwisho baada ya timu mbili, Platinum Stars na Ajax Cape Town kuteremka.
  Baroka ikabaki na pointi zake 34 baada ya kucheza mechi 30, wakati Platinum Stars iliteremka daraja huku Ajax Cape Town ikienda kucheza mechi za mchujo dhidi ya timu zilizoshika nafasi ya pili na ya tatu katika Ligi Daraja la Kwanza ili kuwania bila mafanikio kubaki Ligi Kuu.
  Kikosi cha Baroka FC jana kilikuwa; Elvis Chipezeze, Matome Kgoetyane, Ananias Gebhardt, Abdi Banda, Letladi Madubanya, Bonginkosi Makume/Mduduzi Mdatsane dk77, Talent Chawapiwa/Onkabetse Makgantai dk53, Richard Matloga/Mpho Kgaswane dk59, Ranga Chivaviro, Bheki Maliba na Collins Makgaka.
  Highlands Park; Tapuwa Kapini, Junior Sibande, Sello Glen Motsepe, Luckyboy Mokoena, Denzil Haoseb, Mothobi Mvala, Lindokuhle Mbatha, Lesenya Ramoraka, Ryan Rae, Sabelo Nyembe/Yusuf Bunting dk90, Petrus Ngebo/Thabo Motlafi dk65.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TIMU YA BANDA YAVUNA POINTI TANO KATIKA MECHI TANO ZA MWANZO LIGI KUU YA AFRIKA KUSINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top